Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama, amepokelewa katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Profesa Alhad Mussa Salum.

Mapokezi hayo (kama ilivyodokezwa hapo juu) yalifanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya JMAT-TAIFA, ambapo pande hizo zilipata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu amani, maridhiano, mshikamano wa kitaifa na kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi Jamii na taasisi za kidini katika kuendelea kuhamasisha jamii kudumisha utulivu, maadili na amani nchini.

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA katika bayani yake alisisitiza kuwa JMAT inaona na inaendelea kuona umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, taasisi za Serikali na Wananchi katika kujenga jamii yenye umoja, maridhiano na amani endelevu.

Your Comment